Yohana Mbatizaji alivaa nguo zilizotengenezwa kwa manyoya ya ngamia na kiunoni mwake alijifunga mkanda wa ngozi; chakula chake kilikuwa nzige na asali mwitu. Watu walimwendea kutoka Yerusalemu, Yudea yote na bonde lote la mto Yordani. Nao walipoungama dhambi zao aliwabatiza katika mto Yordani.

Read full chapter