20 Kwa maana nawaambieni, ikiwa haki yenu haitazidi haki ya waandishi wa sheria na Mafari sayo, hamtaingia katika Ufalme wa mbinguni kamwe.”

Mafundisho Kuhusu Hasira

21 “Mmesikia walivyowafundisha watu wa zamani kwamba, ‘Usiue; na ye yote atakayeua atastahili hukumu.’ 22 Lakini mimi nawaambia kwamba, ye yote atakayemkasirikia ndugu yake atasta hili hukumu; na ye yote atakayemtukana ndugu yake, atashtakiwa katika baraza; na ye yote atakayemwambia ndugu yake, ‘Wewe mjinga,’ atastahili hukumu ya moto wa Jehena.

Read full chapter