Wapendeni Maadui Zenu

43 “Mmesikia kuwa watu zamani walikuwa wakisema, ‘Umpende jirani yako na umchukie adui yako.’ 44 Lakini mimi ninawaambia, wapendeni maadui zenu na waombeeni wanaowatesa, 45 ili mpate kuwa watoto wa Baba yenu aliye mbinguni. Kwa maana yeye huwaanga zia jua lake watu waovu na watu wema; na pia huleta mvua kwa wenye haki na wasio haki.

Read full chapter