27 Ni nani kati yenu ambaye kwa kujihangaisha kwake anaweza kujiongezea hata saa moja zaidi kwenye maisha yake?

28 “Na kwa nini mnahangaikia mavazi? Angalieni maua ya mwi tuni yanavyostawi. Hayafanyi kazi wala hayashoni nguo. 29 Lakini nawaambia, hata mfalme Sulemani katika ufahari wake wote hakuwahi kuvikwa kama mojawapo la maua hayo.

Read full chapter