Lakini ninyi mnapotoa sadaka, fanyeni kwa siri, hata mkono wako wa kushoto usijue mkono wako wa kulia unafanya nini; ili sadaka yako iwe ni siri. Naye Baba yako wa mbinguni anayeona sirini ata kupa thawabu.”

Mafundisho Kuhusu Sala

“Na mnaposali, msiwe kama wanafiki; maana wao wanapenda kusimama na kusali katika masinagogi na kando ya barabara ili waonekane na watu. Nawaambieni kweli, wao wamekwisha kupata tuzo yao.

Read full chapter