10 Au akimwomba samaki atampa nyoka? 11 Ikiwa ninyi mlio waovu mnafahamu jinsi ya kuwapa watoto wenu zawadi nzuri, ni mara ngapi zaidi Baba yenu wa mbinguni atawapa vitu vizuri wale wamwombao? 12 Kwa hiyo cho chote ambacho ungependa watu wakutendee, na wewe watendee vivyo hivyo. Hii ndio maana ya sheria ya Musa na Maandiko ya manabii.”

Read full chapter