Njia Nyembamba Na Njia Pana

13 “Ingieni kwa kupitia mlango mwembamba; kwa maana mlango mpana na njia rahisi huelekea kwenye maangamizo, na watu wanaopitia huko ni wengi. 14 Lakini mlango mwembamba na njia ngumu huelekea kwenye uzima, na ni wachache tu wanaoiona.”

Manabii Wa Uongo

15 “Jihadharini na manabii wa uongo wanaowajia wakiwa wamevaa ngozi ya kondoo, kumbe ndani ni mbwa mwitu wakali.

Read full chapter