Manabii Wa Uongo

15 “Jihadharini na manabii wa uongo wanaowajia wakiwa wamevaa ngozi ya kondoo, kumbe ndani ni mbwa mwitu wakali. 16 Mtawatambua kwa matunda yao. Je, unaweza kuchuma zabibu kwenye miiba au tini kwenye michongoma? 17 Vivyo hivyo mti mzuri huzaa matunda mazuri na mti mbaya huzaa matunda mabaya.

Read full chapter