Yesu Aponya Vipofu

27 Yesu alipoondoka pale, vipofu wawili walimfuata wakipiga kelele kwa nguvu, “Mwana wa Daudi, tuhurumie.” 28 Alipoingia ndani wale vipofu walimfuata. Akawauliza, “Mnaamini kwamba ninaweza kuwafanya muone?” Wakamjibu, “Ndio Bwana.” 29 Ndipo Yesu akagusa macho yao akasema, “Na iwe kwenu kama mnavyo amini.”

Read full chapter