33 Na yule pepo alipofukuzwa, yule aliyekuwa bubu aliweza kusema. Ule umati wa watu wakastaajabu, wakasema, “Jambo kama hili halijawahi kuonekana katika Israeli.” 34 Lakini Mafarisayo wakasema, “Huyo anatoa pepo kwa uwezo wa mkuu wa pepo.”

Wafanyakazi Ni Wachache

35 Yesu akazunguka kwenye miji yote na vijiji vyote akifundi sha katika masinagogi na kuhubiri Habari Njema za Ufalme, na kuponya kila ugonjwa na kila udhaifu.

Read full chapter