Paulo Na Barnaba Warudi Antiokia

21 Walipokwisha hubiri Habari Njema katika mji ule na watu wengi wakaamini wakawa wanafunzi, walirudi Listra na Ikonio na Antiokia. 22 Huko waliwatia nguvu wanafunzi na kuwashauri waendelee kukua katika imani. Wakawaonya wakisema, “Tunalazimika kuingia katika Ufalme wa Mungu kwa kupitia katika mateso mengi.” 23 Na baada ya kuwachagulia wazee viongozi katika kila kanisa, wakawakabidhi kwa Bwana waliyemwamini kwa maombi na kufunga.

Read full chapter