25 Na baada ya kufundisha neno la Mungu huko Perga, walikwenda upande wa kusini hadi Atalia. 26 Kutoka huko wakasafiri kwa mashua mpaka Anti okia, ambako walikuwa wameombewa neema ya Mungu kwa kazi ambayo walikuwa wameikamilisha. 27 Walipowasili Antiokia waliwakusanya waamini pamoja wakawaeleza yale yote ambayo Mungu alikuwa amewa tendea, na jinsi Mungu alivyotoa nafasi ya imani kwa watu wasio Wayahudi. 28 Wakakaa huko na wale wanafunzi kwa muda mrefu.

Read full chapter