30 na unyooshe mkono wako ili tuweze kuponya wagonjwa na kutenda ishara na miu jiza kwa jina la mtumishi wako mtakatifu Yesu.” 31 Walipokwisha kusali, nyumba waliyokuwa wamekutania ikatikisika na wote wakaja zwa na Roho Mtakatifu, wakahubiri neno la Mungu kwa ujasiri. 32 Waamini wote walikuwa na nia moja na moyo mmoja, wala hakuna aliyeona mali aliyokuwa nayo kuwa yake, bali walishirikiana vitu vyote kwa pamoja.

Read full chapter