Font Size
Mathayo 12:44-46
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Mathayo 12:44-46
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
44 Inapokosa mahali pa kupumzika, husema, ‘Nitarudi katika nyumba niliyotoka.’ Inaporudi, ikakuta nyumba hiyo bado ni tupu, ikiwa safi na nadhifu, 45 hutoka nje na kuleta roho zingine saba zilizo chafu zaidi yake. Huingia na kuishi humo, na mtu huyo anakuwa na matatizo mengi kuliko mwanzo wakati roho chafu moja iliishi ndani yake. Ndivyo ilivyo kwa kizazi hiki cha watu wanaoishi leo.”
Wafuasi wa Yesu ni Familia Yake Halisi
(Mk 3:31-35; Lk 8:19-21)
46 Yesu alipokuwa akiongea na watu, mama yake na ndugu zake walikuwa nje. Walitaka kuongea naye.
Read full chapter
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
© 2017 Bible League International