Font Size
Mathayo 3:10-12
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Mathayo 3:10-12
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
10 Shoka limewekwa tayari kukata shina la mti katika mizizi yake. Kila mti[a] usiozaa matunda mazuri utakatwa vivyo hivyo na kutupwa motoni.
11 Mimi ninawabatiza kwa maji kuonesha kuwa mmebadilika mioyoni mwenu na pia maishani mwenu. Lakini yupo mwingine ajaye baada yangu, mwenye nguvu zaidi kuliko mimi, huyo atafanya mengi zaidi yangu. Nami niliye mtumwa wa chini kabisa sistahili hata kuinama na kufungua kamba za viatu vyake. Yeye huyo atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto. 12 Naye atakuja akiwa tayari kwa ajili ya kuisafisha nafaka. Atatenganisha nafaka nzuri kutoka kwenye makapi,[b] na kisha ataiweka nafaka nzuri kwenye ghala yake. Kisha atayachoma makapi kwa moto usiozimika.”
Read full chapter
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
© 2017 Bible League International