Add parallel Print Page Options

Ninajua mnachofikiri. Mnataka akasema kuwa, ‘lakini Ibrahimu ni baba yetu!’ Hiyo haijalishi. Ninawaambia Mungu anaweza kumzalia Ibrahimu watoto kutoka katika mawe haya. 10 Shoka limewekwa tayari kukata shina la mti katika mizizi yake. Kila mti[a] usiozaa matunda mazuri utakatwa vivyo hivyo na kutupwa motoni.

11 Mimi ninawabatiza kwa maji kuonesha kuwa mmebadilika mioyoni mwenu na pia maishani mwenu. Lakini yupo mwingine ajaye baada yangu, mwenye nguvu zaidi kuliko mimi, huyo atafanya mengi zaidi yangu. Nami niliye mtumwa wa chini kabisa sistahili hata kuinama na kufungua kamba za viatu vyake. Yeye huyo atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.

Read full chapter

Footnotes

  1. 3:10 mti Watu wasiomtii Mungu ni kama “miti” itakayokatwa.