Add parallel Print Page Options

21 Yesu akaendelea kutembea kutoka pale. Akawaona ndugu wengine wawili, Yakobo na Yohana wana wa Zebedayo. Walikuwa kwenye mashua pamoja na Zebedayo baba yao. Walikuwa wakiandaa nyavu zao za kuvulia samaki. Yesu akawaita wamfuate. 22 Mara moja wakaiacha mashua pamoja na baba yao na wakamfuata Yesu.

Yesu Afundisha na Kuponya Watu

(Lk 6:17-19)

23 Yesu alikwenda sehemu zote za Galilaya, akifundisha na akihubiri Habari Njema katika masinagogi kuhusu Ufalme wa Mungu. Aliponya magonjwa yote na madhaifu mengi ya watu.

Read full chapter