Font Size
Mathayo 4:24-25
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Mathayo 4:24-25
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
24 Habari kuhusu Yesu zilienea katika nchi yote ya Shamu, na watu waliwaleta wale wote wenye kuteswa na magonjwa na maumivu mbalimbali. Baadhi yao walikuwa na mashetani, wengine walikuwa na kifafa na wengine walikuwa wamepooza. Yesu akawaponya wote. 25 Makundi makubwa ya watu walimfuata; watu kutoka Galilaya, na jimbo lililoitwa Miji Kumi,[a] Yerusalemu, Yuda na maeneo ng'ambo ya Mto Yordani.
Read full chapterFootnotes
- 4:25 Miji Kumi Jimbo hili lilikuwa mashariki ya Ziwa la Galilaya na wakazi wake hawakuwa Wayahudi. Miji Kumi imejulikana pia kama Dekapoli.
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
© 2017 Bible League International