Font Size
Mathayo 5:23-25
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Mathayo 5:23-25
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
23 Unapokwenda kutoa sadaka yako madhabahuni na ukakumbuka kuwa kuna mtu ana jambo dhidi yako. 24 Unapaswa kuiacha sadaka yako kwenye madhabahu na uende kupatana na mtu huyo. Ukiisha patana naye ndipo urudi na kuitoa sadaka hiyo.
25 Akiwepo mtu anayetaka kukushtaki, patana naye haraka. Jitahidi kufanya hivyo kabla ya kufika mahakamani, hata kama bado mpo njiani. Usipofanya hivyo anaweza kukupeleka kwa hakimu. Na hakimu atakupeleka kwa walinzi watakaokufunga gerezani.
Read full chapter
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
© 2017 Bible League International