Wimbo Wa Ushindi

19 Baada ya haya nikasikia sauti kama sauti kuu ya umati mkubwa wa watu mbinguni ikisema kwa nguvu, “Haleluya! Wokovu na utukufu na uweza ni wa Mungu wetu. Maana hukumu zake ni za kweli na haki, amemhukumu yule kahaba mkuu aliyeuharibu ulimwengu kwa uasherati wake. Mungu amelipiza kisasi kwa ajili ya damu ya watumishi wake.” Kwa mara nyingine wakasema kwa nguvu, “Hale luya! Moshi wake huyo kahaba unapanda juu milele na milele.”

Read full chapter