Font Size
Ufunua wa Yohana 7:1-3
Neno: Bibilia Takatifu
Ufunua wa Yohana 7:1-3
Neno: Bibilia Takatifu
Watu 144,000 Wawekewa Muhuri
7 Baada ya haya nikaona malaika wanne wamesimama katika pembe zote nne za dunia wakizuia pepo nne za dunia, ili upepo usivume nchi kavu wala baharini wala kwenye mti wo wote. 2 Kisha nikaona malaika mwingine akija kutoka mashariki akiwa na muhuri wa Mungu aliye hai. Akawaita kwa sauti kuu wale malaika waliokuwa wamepewa mamlaka kuidhuru nchi na bahari, akisema, 3 “Msiidhuru nchi wala bahari, wala miti, mpaka tutakapoweka mihuri kwenye vipaji vya nyuso za watumishi wa Mungu wetu.”
Read full chapter
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Copyright © 1989 by Biblica