Kisha nikaona malaika mwingine akija kutoka mashariki akiwa na muhuri wa Mungu aliye hai. Akawaita kwa sauti kuu wale malaika waliokuwa wamepewa mamlaka kuidhuru nchi na bahari, akisema, “Msiidhuru nchi wala bahari, wala miti, mpaka tutakapoweka mihuri kwenye vipaji vya nyuso za watumishi wa Mungu wetu.”

Ndipo nikasikia idadi ya wale waliowekewa mihuri, watu 144,000 kutoka katika kila kabila la Waisraeli.

Read full chapter