Tarumbeta Ya Sita

13 Malaika wa sita akapiga tarumbeta yake, nami nikasikia sauti ikitoka katika zile pembe nne za madhabahu iliyoko mbele ya Mungu. 14 Sauti hiyo ikamwambia yule malaika wa sita mwenye tar umbeta, “Wafungulie wale malaika wanne waliofungwa kwenye mto mkubwa wa Efrati.” 15 Basi wakafunguliwa wale malaika wanne waliokuwa wamewekwa tayari kwa ajili ya saa hiyo, na siku hiyo na mwezi huo na mwaka huo, wawaue theluthi moja ya wanadamu.

Read full chapter