15 Basi wakafunguliwa wale malaika wanne waliokuwa wamewekwa tayari kwa ajili ya saa hiyo, na siku hiyo na mwezi huo na mwaka huo, wawaue theluthi moja ya wanadamu. 16 Idadi ya majeshi wapandao farasi ilikuwa milioni mia mbili. 17 Na hivi ndivyo nilivyowaona hao farasi na wapanda farasi katika maono yangu: wapanda farasi walivaa ngao vifuani zenye rangi ya moto na samawati na kiberiti. Na vichwa vya farasi hao vilikuwa kama vichwa vya simba; na moto, moshi na kiberiti vili kuwa vinatoka vinywani mwao.

Read full chapter