Add parallel Print Page Options

19 Walirusha mavumbi juu ya vichwa vyao na kulia kwa sauti kuu kuonesha huzuni kuu waliyokuwa nayo. Walisema:

“Inatisha! Inatisha sana kwa mji mkuu!
    Wote waliokuwa na meli baharini walitajirika kwa sababu ya utajiri wake!
    Lakini umeteketezwa katika saa moja!
20 Ufurahi kwa sababu ya hili, Ee mbingu!
    Furahini, watakatifu wa Mungu, mitume na manabii!
Mungu amemhukumu kwa sababu ya kile alichowatendea ninyi.”

21 Kisha malaika mwenye nguvu akainua jiwe kubwa. Jiwe hili lilikuwa kubwa kama jiwe kubwa la kusagia. Malaika akalitupia jiwe baharini na kusema:

“Hivyo ndivyo mji mkuu Babeli utakavyotupwa chini.
    Hautaonekana tena.

Read full chapter