Add parallel Print Page Options

11 Kisha kila mmoja wao alipewa kanzu ndefu nyeupe. Wakaambiwa wasubiri kwa muda mfupi kwani bado walikuwepo ndugu zao katika utumishi wa Kristo ambao ni lazima wauawe kama wao. Roho hizi ziliambiwa zisubiri mpaka mauaji yote yatakapokwisha.

12 Kisha nilitazama wakati Mwanakondoo anaufungua muhuri wa sita. Kulitokea tetemeko kubwa la ardhi na jua likawa jeusi kama gunia jeusi[a] na mwezi wote ukawa mwekundu kama damu. 13 Nyota zikaanguka chini duniani kama mtini uangushavyo tini zake upepo unapovuma.

Read full chapter

Footnotes

  1. 6:12 gunia jeusi Gunia lililofumwa kwa nyuzi za manyoya maeusi.