Add parallel Print Page Options

12 Kisha nilitazama wakati Mwanakondoo anaufungua muhuri wa sita. Kulitokea tetemeko kubwa la ardhi na jua likawa jeusi kama gunia jeusi[a] na mwezi wote ukawa mwekundu kama damu. 13 Nyota zikaanguka chini duniani kama mtini uangushavyo tini zake upepo unapovuma. 14 Anga iligawanyika katikati na pande zote zikajiviringa kama kitabu.[b] Na kila mlima na kisiwa kiliondolewa mahali pake.

Read full chapter

Footnotes

  1. 6:12 gunia jeusi Gunia lililofumwa kwa nyuzi za manyoya maeusi.
  2. 6:14 kitabu Hapa inamaanisha hati ndefu ya kukunja kwa kuvingirisha (vitabu vilivyotumika zamani). Katika Biblia unapoona neno kitabu au vitabu, inamaanisha hati hizi.