Font Size
Ufunuo 8:10-12
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Ufunuo 8:10-12
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
10 Malaika wa tatu alipopuliza tarumbeta yake. Nyota kubwa, inayowaka kama tochi ikaanguka kutoka mbinguni. Ilianguka kwenye theluthi moja ya mito na chemichemi za maji. 11 Jina la nyota hiyo lilikuwa Uchungu.[a] Na theluthi moja ya maji yote yakawa machungu. Watu wengi wakafa kutokana na kunywa maji haya machungu.
12 Malaika wa nne alipopuliza tarumbeta yake. Theluthi ya jua, theluthi ya mwezi na theluthi ya nyota vikapigwa. Hivyo theluthi moja yao vikawa giza. Theluthi moja ya mchana na usiku ikakosa mwanga.
Read full chapterFootnotes
- 8:11 Uchungu Kwa maana ya kawaida, “mti mchungu”, mti mchungu sana; hapa, inaashiria huzuni yenye uchungu mwingi.
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
© 2017 Bible League International