Add parallel Print Page Options

11 Jina la nyota hiyo lilikuwa Uchungu.[a] Na theluthi moja ya maji yote yakawa machungu. Watu wengi wakafa kutokana na kunywa maji haya machungu.

12 Malaika wa nne alipopuliza tarumbeta yake. Theluthi ya jua, theluthi ya mwezi na theluthi ya nyota vikapigwa. Hivyo theluthi moja yao vikawa giza. Theluthi moja ya mchana na usiku ikakosa mwanga.

13 Nilipokuwa ninatazama, nilimsikia tai aliyekuwa anaruka juu sana angani akisema kwa sauti kuu, “Ole! Ole! Ole kwa wale wanaoishi duniani! Shida kuu zitaanza baada ya sauti za tarumbeta ambazo malaika wengine watatu watapuliza.”

Read full chapter

Footnotes

  1. 8:11 Uchungu Kwa maana ya kawaida, “mti mchungu”, mti mchungu sana; hapa, inaashiria huzuni yenye uchungu mwingi.