Font Size
Ufunuo 9:1-3
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Ufunuo 9:1-3
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Tarumbeta ya Tano Yaanzisha Kitisho cha Kwanza
9 Malaika wa tano alipopuliza tarumbeta yake, niliiona nyota ikianguka kutoka angani mpaka duniani. Nyota ilipewa ufunguo wa kufungulia shimo refu sana liendalo kuzimu. 2 Kisha nyota ikafungua shimo refu sana liendalo kuzimu. Moshi ukatoka kwenye shimo kama moto utokao kwenye tanuru kubwa. Jua na anga vikawa giza kwa sababu ya moshi uliotoka kwenye shimo.
3 Nzige wakatoka kwenye moshi na wakateremka kwenda duniani. Walipewa nguvu ya kuuma kama nge.
Read full chapter
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
© 2017 Bible League International