16 Msiache kutenda mema na kushirikiana mlivyo navyo, kwa maana sadaka kama hizi ndizo zinazompendeza Mungu.

17 Watiini viongozi wenu na kufanya wanavyowaagiza. Wao wanachunga roho zenu, kama watu ambao watatoa ripoti ya huduma yao. Watiini kusudi wafanye kazi yao kwa furaha, na wala si kama mzigo, maana hiyo haitakuwa na faida kwenu.

18 Tuombeeni, kwa maana tuna hakika kwamba tunayo dhamiri safi na tunapenda kufanya yaliyo sawa daima.

Read full chapter