Font Size
Waefeso 3:6-8
Neno: Bibilia Takatifu
Waefeso 3:6-8
Neno: Bibilia Takatifu
6 Siri hii ni kwamba, kwa njia ya Injili, watu wa mataifa ni warithi pamoja na Waisraeli; na wote pamoja ni viungo vya mwili mmoja, na ni washiriki kwa pamoja wa ile ahadi aliyotoa Mungu katika Kristo Yesu. 7 Niliteuliwa kuwa mtumishi wa Injili hii kwa kipawa cha neema ya Mungu niliyopewa kwa uwezo wake uliokuwa ukifanya kazi ndani yangu. 8 Ingawa mimi ni mdogo kuliko hata aliye mdogo kabisa kati ya watu wote wa Mungu, nilipewa neema hii, niwahubirie watu wa mataifa kuhusu utajiri usiopimika ulio ndani ya Kristo.
Read full chapter
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Copyright © 1989 by Biblica