10 ili mpate kutambua mambo yaliyo mema. Na pia mpate kuwa watu safi, wasio na hatia hadi siku ya Kristo. 11 Maisha yenu yawe na matunda ya haki yatokayo kwa Yesu Kristo, ili Mungu apewe utukufu na sifa. 12 Ndugu zangu, napenda mfahamu kwamba haya mambo yaliyonipata yamesaidia sana kueneza Injili ya Kristo.

Read full chapter