20 Kwa hiyo hakuna binadamu hata mmoja atakayehesabiwa kuwa na haki mbele za Mungu kwa kufuata sheria; bali sheria hutufanya tutambue dhambi.

Haki Kwa Njia Ya Imani

21 Lakini sasa, njia ya Mungu ya kuwahesabia watu haki pasipo sheria, njia ambayo sheria na manabii huishuhudia, imekwisha dhihirishwa. 22 Haki hii itokayo kwa Mungu hupatikana kwa kumwaminiYesu Kristo. Mungu huwatendea hivi watu wote wamwa minio Kristo pasipo kubagua,

Read full chapter