Add parallel Print Page Options

Mungu Anavyowafanya Watu Kuwa Wenye Haki

21 Lakini sasa Mungu ametuonesha jinsi alivyo mwema na mwaminifu. Alivyofanya haihusiani na sheria ingawa sheria na manabii walisema kuwa haya yangetokea. 22 Uaminifu wa wema wa Mungu umedhihirishwa kwetu kupitia imani katika[a] Yesu Kristo. Hufanya hivi kwa wote wanaomwamini Kristo. Kwa sababu kwa Mungu watu wote ni sawa. 23 Ndiyo, watu wote wametenda dhambi na wameshindwa kufikia kiwango cha utukufu wa Mungu kilichokusudiwa kwao.

Read full chapter

Footnotes

  1. 3:22 imani katika Au “uaminifu wa”.