Add parallel Print Page Options

22 Uaminifu wa wema wa Mungu umedhihirishwa kwetu kupitia imani katika[a] Yesu Kristo. Hufanya hivi kwa wote wanaomwamini Kristo. Kwa sababu kwa Mungu watu wote ni sawa. 23 Ndiyo, watu wote wametenda dhambi na wameshindwa kufikia kiwango cha utukufu wa Mungu kilichokusudiwa kwao. 24 Mungu ameamuru sisi sote tufunguliwe kutoka dhambini. Zawadi hii ya neema yake imekuja kwetu kupitia kile ambacho Kristo Yesu alikifanya ili tuwe huru.

Read full chapter

Footnotes

  1. 3:22 imani katika Au “uaminifu wa”.