23 kwa maana wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; 24 wote wanahesabiwa haki bure kwa neema yake kwa ukombozi ulioletwa na Yesu Kristo. 25 Mungu alimtoa awe dhabihu ya upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake. Alifanya hivi ili kuonyesha haki yake, kwani kwa uvumilivu wake hakuziadhibu dhambi za zamani.

Read full chapter