La hasha! Mun gu ana haki kabisa kutughadhibikia! Kama sivyo, Mungu angewezaje kuuhukumu ulimwengu? Mtu anaweza kusema,“Kama uongo wangu unasaidia kuonyesha ukweli wa Mungu na hivyo kudhihirisha utukufu wake, kwa nini basi ninahukumiwa kama mwenye dhambi?” Kwa nini tusiseme, kama wengine wanavyotusingizia kuwa tunasema, “Tutende maovu ili wema udhihirike”? Hakika hukumu wanayoipata ni ya haki.

Read full chapter