Mtu anaweza kusema,“Kama uongo wangu unasaidia kuonyesha ukweli wa Mungu na hivyo kudhihirisha utukufu wake, kwa nini basi ninahukumiwa kama mwenye dhambi?” Kwa nini tusiseme, kama wengine wanavyotusingizia kuwa tunasema, “Tutende maovu ili wema udhihirike”? Hakika hukumu wanayoipata ni ya haki.

Wote Wametenda Dhambi

Tusemeje basi? Sisi Wayahudi tunayo nafuu yo yote? Hata kidogo! Kama tulivyokwisha kusema, Wayahudi na Wagiriki, wote wanatawaliwa na nguvu ya dhambi.

Read full chapter