Add parallel Print Page Options

17 Kila karama njema na kila tuzo kamilifu hutoka juu; hushuka chini kutoka kwa Baba aliyeumba nuru zote zilizoko mawinguni ambamo kwake yeye hakuna mabadiliko kama vile vivuli vinavyosababishwa na mzunguko wa sayari. 18 Kwa uamuzi wake mwenyewe Mungu alituzaa sisi na kuwa watoto wake kwa njia ya ujumbe wa kweli ili tuwe mazao ya kwanza[a] yenye heshima ya pekee miongoni mwa vyote alivyoviumba.

Kusikiliza na Kutii

19 Kumbukeni hili ndugu zangu wapendwa: Kila mtu awe mwepesi wa kusikia lakini awe mzito wa kusema, na mzito kukasirika,

Read full chapter

Footnotes

  1. 1:18 mazao ya kwanza Kwa Waisraeli “mazao ya kwanza” yalikuwa sehemu ya kwanza ya mazao ambayo walileta kwa Kuhani kwa ajili ya kumtolea Mungu. Paulo amelitumia neno hili kwa kanisa. Hapa neno hili limetumika kwa maana ya heshima maalumu ambayo waaminio wanayo mbele ya Mungu tofauti na viumbe vyote. Hawa wanategemea uumbaji mpya na ukombozi ambao wanadamu watakutana nao katika mbingu mpya.