Font Size
Yakobo 1:18-20
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Yakobo 1:18-20
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
18 Kwa uamuzi wake mwenyewe Mungu alituzaa sisi na kuwa watoto wake kwa njia ya ujumbe wa kweli ili tuwe mazao ya kwanza[a] yenye heshima ya pekee miongoni mwa vyote alivyoviumba.
Kusikiliza na Kutii
19 Kumbukeni hili ndugu zangu wapendwa: Kila mtu awe mwepesi wa kusikia lakini awe mzito wa kusema, na mzito kukasirika, 20 kwa sababu hasira ya mwanadamu haitoi haki inayohitajiwa na Mungu toka kwetu.
Read full chapterFootnotes
- 1:18 mazao ya kwanza Kwa Waisraeli “mazao ya kwanza” yalikuwa sehemu ya kwanza ya mazao ambayo walileta kwa Kuhani kwa ajili ya kumtolea Mungu. Paulo amelitumia neno hili kwa kanisa. Hapa neno hili limetumika kwa maana ya heshima maalumu ambayo waaminio wanayo mbele ya Mungu tofauti na viumbe vyote. Hawa wanategemea uumbaji mpya na ukombozi ambao wanadamu watakutana nao katika mbingu mpya.
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
© 2017 Bible League International