Font Size
Yohana 10:27-29
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Yohana 10:27-29
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
27 Kondoo wangu huisikia sauti yangu. Nami nawajua, nao hunifuata. 28 Mimi nawapa kondoo wangu uzima wa milele. Nao hawatakufa kamwe, na tena hakuna atakayemchukua yeyote kutoka mkononi mwangu. 29 Baba yangu ndiye aliyenipa hao, naye ni mkuu kuliko wote.[a] Hakuna anayeweza kuwaiba kondoo wangu kutoka mkononi mwangu.
Read full chapterFootnotes
- 10:29 Baba yangu … kuliko wote Baadhi ya nakala za zamani za Kiyunani zina, “Kile ambacho Baba amenipa ni kikubwa kuliko vyote.” Kuna tafsiri nyingi katika makala za zamani za Kiyunani. Nakala zingine za baadaye zina “Baba yangu, ambaye amewapa kwangu mimi ni mkuu kuliko wote.”
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
© 2017 Bible League International