Yesu Anawaombea Wanafunzi Wake

17 Yesu alipomaliza kusema maneno haya, alitazama mbinguni akasema, “Baba, wakati umefika. Dhihirisha utukufu wangu ili nami nikutukuze wewe, kwa kuwa umenipa mamlaka juu ya watu wote, niwape uzima wa milele wale ambao umewakabidhi kwangu. Na huu ndio uzima wa milele: wakufahamu wewe ambaye pekee ni Mungu wa kweli, nakumfah amu Yesu Kristo ambaye umemtuma.

Read full chapter