Sasa wamefahamu ya kuwa vyote ulivyonipa vinatoka kwako ; kwa kuwa nimewapa ujumbe ulionipa, nao wameupokea. Wamefahamu hakika ya kuwa nimetoka kwako na wameamini kwamba ulinituma. Siwaombei watu wote wa ulimwengu bali nawaombea hawa ulionipa kwa sababu wao ni wako.

Read full chapter