Siwaombei watu wote wa ulimwengu bali nawaombea hawa ulionipa kwa sababu wao ni wako. 10 Wote ulionipa ni wako, na walio wako ni wangu; nao wanadhihirisha utukufu wangu. 11 Mimi naondoka ulimwenguni ninakuja kwako. Lakini wao wako ulimwenguni. Baba Mtakatifu, walinde kwa jina lako ambalo umenipa ili wawe na umoja kama sisi tulivyo mmoja.

Read full chapter