Simoni Petro aka waambia wenzake, “Mimi nakwenda kuvua samaki.” Nao wakamwambia, “Tutakwenda pamoja nawe.” Wakatoka, wakaingia ndani ya mashua. Lakini usiku ule hawakupata cho chote. Kulipopambazuka, Yesu alisimama ufukoni, lakini wale wana funzi hawakumtambua. Yesu akawaambia, “Wanangu, mmepata samaki wo wote?” Wakamjibu, “La.”

Read full chapter