10 Yesu akamjibu, “Kama ungelifahamu Mungu anataka kukupa nini, na mimi ninayekuomba maji ya kunywa ni nani, ungeliniomba nikupe maji ya uzima.”

11 Yule mwanamke akamjibu, “Bwana, wewe huna chombo cha kuchotea maji na kisima hiki ni kirefu . Hayo maji ya uzima utay apata wapi? 12 Kwani wewe ni mkuu kuliko baba yetu Yakobo ambaye alitupatia kisima hiki, ambacho yeye pamoja na watoto wake na mifugo yake walikitumia?”

Read full chapter