Add parallel Print Page Options

Yesu ni Neno la Mungu la Milele

Mwanzoni Kabla ulimwengu haujaumbwa
    alikuwepo Neno.[a]
Huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu,
    na Neno alikuwa Mungu.
Alikuwepo pamoja na Mungu
    toka mwanzo.
Kila kitu kilifanyika kupitia kwake.
    Hakuna chochote katika uumbaji wa Mungu
    kilichofanyika bila yeye.
Ndani yake Neno kulikuwemo na uzima,
    na uzima huo ulikuwa nuru
    kwa ajili ya watu wa ulimwenguni.
Nuru[b] hiyo yamulika gizani,
    na giza halikuishinda.[c]

Alikuwepo mtu aliyeitwa Yohana, aliyetumwa na Mungu. Alikuja kuwaambia watu kuhusu nuru. Ili kupitia kwake watu wote waweze kusikia kuhusu yule aliye nuru na wamwamini. Yohana mwenyewe hakuwa nuru. Lakini alikuja kuwaambia watu kuhusu nuru.

Nuru ya kweli,
    anayeleta mwangaza kwa watu wote,
    alikuwa tayari kuonekana kwa ulimwengu.

Read full chapter

Footnotes

  1. 1:1 Neno Kwa Kiyunani neno hili ni logos, lenye maana mawasiliano ya aina yoyote. Linaweza kutafsiriwa “ujumbe”. Hapa lina maana ya Kristo; njia ambayo Mungu alitumia kuueleza ulimwengu kuhusu yeye. Pia katika mstari wa 10,14 na 16.
  2. 1:5 Nuru Lenye maana ya Kristo, Neno, aliyeleta ulimwenguni uelewa kuhusu Mungu. Pia katika mstari wa 7.
  3. 1:5 halikuishinda Au “kupotosha ukweli”.