Add parallel Print Page Options

23 Mmezaliwa upya sio kama matokeo ya mbegu inayoharibika, lakini kama matokeo ya mbegu isiyoharibika. Mmezaliwa upya kwa njia ya ujumbe wa Mungu, ambao unaleta uzima ndani yenu. 24 Hivyo, kama Maandiko yanavyosema:

“Watu wote ni kama manyasi,
    na utukufu wao wote ni kama maua pori katika manyasi.
Manyasi yananyauka na kukauka,
    na maua yanapukutika,
25     bali ujumbe wa Bwana unadumu milele.”(A)

Na ujumbe huo ni habari njema iliyohubiriwa kwenu.

Read full chapter