Kuwatii Wenye Mamlaka

13 Jinyenyekezeni kwa ajili ya Bwana chini ya mamlaka yote ya wanadamu: ikiwa ni mfalme ambaye ana mamlaka ya mwisho; 14 au ikiwa ni wakuu wengine ambao amewateua kuwaadhibu wahalifu na kuwasifu watendao mema. 15 Kwa maana ni mapenzi ya Mungu kwamba kwa kutenda mema myazime maneno ya kijinga ya watu wapumbavu.

Read full chapter